Skip to main content

Mganga Ajabu Wa Au, sura ya kwanza

MGANGA AJABU WA AU

1. Kimbuga

Dorothy aliishi katikati mwambuga kubwa huko Kansas na mjombake Henry aliyekuwa mkulima, pamoja naye shangaziye Em aliyekuwa mkewe mkulima. Nyumba yao ilikuwa ndogo,kwa sababu mbao zilizotumiwa kuitengeneza ilibidi zibebwe maili nyingi. Kulikuwa na kuta nne, sakafu na paa, zilizounda chumba kimoja; chumba hiki kilikuwa na jiko iliyokuwa imejaa kutu, kabati palipowekwa sahani, meza, viti vitatu au vinne, na vitanda.
Mjomba Henri na shangazi Em walikuwa na jitanda kona moja, naye Dorothy kijitanda kona nyingine. Hapakuwa na $$$$ hata, pia hapakuwa na $$$ isipokuwa shimo ndogo iliyochimbwa ardhini, iliyoitwa $$$ ya kimbuga, mahali ambapo familia ingekimbia kama mojawapo wa upepo mkubwa ungezuka , iliyokuako kubwa kubwa kiasi cha kuvunja na kuharibu nyumba yoyote pahali popote ilipopita. Ili uingie $$$ ya limbuga ulifungua mlango mdogo katikati mwa sakafu, ambapo palikuwa na ngazi iliyoshuka mpaka ndani mwa shimo hii ndogo iliyokuwa na giza.
Dorothy aliposimama mlangoni na kutazama kila mahali hakuona chochote isipokuwa mbuga kubwa yenye rangi ya kijijivu kila upande. Kila mahali ulipotazama hapakuwa na mti wala nyumba mpaka zilipokutana mbingu na ardhi. Ardhi yote iliyokuwa imetifuliwa ilikuwa imechomwa na jua na kushikamana na kuwa rangi ya kijivujivu ikiwa imepasuka pasuka.Hata nyasi nayo haikuwa rangi ya kijani, kwani ilikuwa imecnomwa na jua na kuwa rangi ya kijivujivu kama ilivyokuw kila mahali. Kitambo nyumba ilikuwa imepakwa rangi, lakini jua na mvua ziliungana na kuisafisha nyumba pia ikawa rangi isiyovutia, rangi ya kijivujivukama kila kitu kingine.
Shangazi Em alipokuja kuishi hapa alikuwa mke mrembo sana. Jua na upepo zilikuwa zimembadilisha pia yeye. Macho yake yaliacha kuvutia ikawa pia rangi hii ya kijivujivu; uso wake wote ulibadilika na kuwa rangi hii mbaya. Alionekana amishiwa na nguvu na akawa tu mifupa na akiwacha kucheka siku hizi. Dorothy, ambaye alikuwa ni yatima, alipokuja kuishi naye, Shangazi Em alishinda akiwika mara kwa mara Dorothy alipocheka. Mambo haya yalimshangaza sana, alishindwa mtoto huyu allikuwa akifurahishwa na nini kila wakati.
Mjomake Henri hakucheka hata. Alifanya kazi asubuhi mpaka usiku na hakujua furaha ilikuwa nini. Pia yeye alikuwa na rangi hii ya kijivujivu, kutoka kwa machavu mpaka kwa viatu vyake, alionekana mwenye fikira na huzuni na alisema kidogo.
Toto ndiye aliyemfanya Dorothy acheke ana alimzuia kubadilika rangi na kuwa kama mazingira yake. Toto hakuwa mwenye rangi ya kijivujivu; alikuwa mbwa mdogo mwenye rangi nyeusi na nywele ndefu laini kama $$$, alikuwa na macho madogo nyeusi yaliyomeremeta kila upande wa pua lake ndogo. Toto alishinda akicheza siku nzima na Dorothy alicheza naye, na alimpenda sana.
Leo lakini hawakuwa wakicheza. Henry mjombake alikaa mlangoni na kutazama mbingu na matarajio$$$$ iliyokuwa imebadilika na kuwa na rangi ya kujijivu kuliko kawaida. Dorothy alisimama mlangoni na kutazama mbingu pia akiwa amemshika toto mkononi. Em shangaziye alikuwa akiosha sahani.
Kutoka kaskazini walisikia mlio wa upepo kwa umbali, Dorothy an mjombake Hneri waliweza kuona nyasi ikiinama kutokana na upepo mkali ulikuwa ukija. Pakawa sauti kubwa hewani kutoka kusini, wakatazama nyuma wakona pia nyasi ilikuwa pia ikiinama vivyo hivyo.
Ghafla Henri mjombake akasimama.
" Kimbuga cha kuja Em," alimwita mkewe. " nitaenda kuichunga mifugo" Kisha akakimbia zizini walipowekwa ngombe na farasi.
Em shangaziye akaacha kazi yake akakimbia mlangoni. alitazama tu na akajua hatari iliyokuwa ikija.
"Dorothy kimbia!" aliwika. "kimbia uingie kwenye shimo la kimbuga!"
Toto aliruka kutoka mikononi mwa Dorothy na kukimbia akajicha chini ya kitanda, naye msichana akenda kumtafuta.Em, aliyekuwa amepatwa na mshangao mkubwa alilifungua lango lilokuwa sakafuni na kushuka kwa ngazi mpaka ndani ya shimo iliyokuwa na giza.
Dorothy hatimaye aliweza kumshika mbwa wake Toto na akaanza kumfuata shangaziye. Alipokuwa ametembea na kufika nusu ya chumba pakawa na kilio kikubwa cha upeponalo nyumba nzima likatingizika kwa kishindo mpaka Dorothy akateleza na kuanguka na kukaa kwa ghafla sakafuni. Kisha kitu cha kustaajabisha kikafanyika. Nyumba ikazunguka mara mbili tatu na ikaanza kupaa hewani. Dorothy akajihisi kama alikuwa akipaa ndani ya puto. Zilipokutana pepo kutoka kaskazini na kusini ndipo nyumba ilipokuwa imesimama na hapa pakawa katikati mwa kimbuga. Ndani katikati mwa kimbuga huwa pametulia, lakini uzito na nguvu ya upepo uliokuwa pande zote za nyumba ulilibeba nyumba juu mpaka likafika juu ya kimbuga; na hapo likabaki na likabebwa kilimita nyingi kwa urahisi kama karatasi/nyoya.
Palikuwa na giza , upepo ulivuma kwa ukali pande zake zote, lakini dorothy aliona ya kuwa aliweza kupaa kwa urahisi.Baada ya muda wa kwanza juu hewani, kuzungushwa na upepona mara myingine moja nyumba ilipopinduka vibaya, alihisi kama mtoto mchanga anavyobebelezwa kitandani. Toto hakuipenda hataa. Alishinda akikimbia, mara hako hapa mara ako pale kote chumbani, akibweka kwa nguvu; lakini dorothy alikaa chini amenyamaza kimya kwenye sakafu akiterejea kitakachofanyika.
Wakati mmoja Toto alikaribia palipokuwa na shimo sakafuni, penye lango, na kuanguka ndani; Dorothy akadhani amempoteza. Lakini baada ya muda mfupi aliliona sikio moja lake likichomoza kutoka kwa shimo, nguvu ya upepo ilimzuia kuanguka kwani ilimpuliza juu. Dorothy alitambaa mpaka shimoni na kumshika Toto kwa sikio na kumvuta ndani ya chumba kisha akalifunga lango kuzuia ajali nyingine kufanyika.
Masaa ikapita, na baada ya muda dorothy aliwacha kuogopa lakini alipatwa na hisia za upweke. Sauti kubwa ya upepo ilitishia kumfanya kiziwi. Mwanzoni alidhania ataangushwa chini kama nyungu na kuwa vipande nyumba ilipoanguka chini tena; lakini masaa yalipozidi kupita na hakuna lolote mbaya lililofanyika, aliwacha kuwa na masikitiko na akaamua kungoja kama ametulia na kungoja yatakayokuja. Mwishowe alitambaa juu ya sakafu iliyokuwa ikitingizika mpaka kitandani na akalala juu yake nae toto alimfuata na kulala kando yake. Hata ingawa nyumba ilikuwa ikitingizika na upepo ulivuma kwa kelele baada ya muda dorothy alifunga macho yake na akalala usingizi mnono.

Comments

Popular posts from this blog

Swahili translation of the Wonderful Wizard of Oz

Hii ni tafsiri ya kitabu cha L. Frank Baum, The Wonderful Wizard of Oz. Jina lake baada ya kufikiri na kuchunguza maana ya Oz nimeona katika kiswahili ,"Mganga Ajabu Wa Au." Oz lilitokana na ufupisho wa neno Ounce  ambacho ni kipimo cha dhahabu, Kwa ksiwahili ni Aunsi nami nikafupisha likawa Au, ambayo imenipa Mganga Au. I will publish a chapter by chapter of the whole book. Copyright 2011

SURA YA KWANZA HADI YA TATU.

Utangulizi     Ngano. masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu jadi. Kila mtoto mdogo mwenye afya anazipenda kwa moyo wake wote hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu. Fari zenye bawa, zilizobuniwa nao Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya watoto kuliko hadithi zote alizobuni mwanadamu.     Lakini hadithi hizi zinazohusu fari, zilizohudumuia vizazi sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ katika maktaba ya watoto; wakati umefika kwa hadithi mpya za ajabu nazo zile zilizoeleka za jini,dwafu na fari kuondolewa, pamoja na mambo yote ya kutisha yaliyowekwa na watungaji hadithi ili kutoa funzo. Elimu ya kisasa inawapa watoto maadili; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake. Mtoto huyu anatupilia mbali kwa furaha vitukio vyote asivyokubaliana navyo.     Tukiwa na fikra hizi akilini, hadithi ya “ Mganga Ajabu wa Au” iliandikwa kwa lengo moja tu la kuwafurahisha watoto wa siku hii. Hadithi hii inalenga kuwa