Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2011

Mganga Ajabu Wa Au, Sura ya Pili

2. Kongamano la Dorothy na Watu wa Kushangaza. Aliamshwa na kishindo kikubwa dorothy asingalikuwa amelala kitandani angeumia. navyo ilivyokuwa kishindo kilimfanya astaajabu na kufikiri kilichofanyika; naye Toto akiiweka pua yake baradi usoni mwake dorothy na whined dismally. Dorothy aliamka na akangalia kila mahali. Nyumba ilikuwa imewacha kusonga; na pia sasa hapakuwa na giza, kwani jua lilikuwa likiwaka kupitia kioo, kujaza chumba chote. Dorothy alitoka kitandani naye toto akimfuata nyuma akiimbia na akaenda akalifungua mlango. Msichana mdogo aliwika kwa furaha kwa sababu ya mambo yote ya ajabu aliyoyaona macho yake yakipanuka yakawa kubwa kama sahani. Kimbuga kilikuwa kimeitua nyumba kwa utulivu- kwa kimbuga- katika nchi ya urembo tele. Palikuwa na nyasi yenye rangi ya kijani kibichi nayo miti ilikuwa kubwa na iliyokuwa na matunda makubwa yalionekana tamu sana.Kulikuwa na maua chungu nzima kila mahali alipotazama, ndege wenye rangi ambazo ahakuwahi kuona maisha yake yote yen

Mganga Ajabu Wa Au, sura ya kwanza

MGANGA AJABU WA AU 1. Kimbuga Dorothy aliishi katikati mwambuga kubwa huko Kansas na mjombake Henry aliyekuwa mkulima, pamoja naye shangaziye Em aliyekuwa mkewe mkulima. Nyumba yao ilikuwa ndogo,kwa sababu mbao zilizotumiwa kuitengeneza ilibidi zibebwe maili nyingi. Kulikuwa na kuta nne, sakafu na paa, zilizounda chumba kimoja; chumba hiki kilikuwa na jiko iliyokuwa imejaa kutu, kabati palipowekwa sahani, meza, viti vitatu au vinne, na vitanda. Mjomba Henri na shangazi Em walikuwa na jitanda kona moja, naye Dorothy kijitanda kona nyingine. Hapakuwa na $$$$ hata, pia hapakuwa na $$$ isipokuwa shimo ndogo iliyochimbwa ardhini, iliyoitwa $$$ ya kimbuga, mahali ambapo familia ingekimbia kama mojawapo wa upepo mkubwa ungezuka , iliyokuako kubwa kubwa kiasi cha kuvunja na kuharibu nyumba yoyote pahali popote ilipopita. Ili uingie $$$ ya limbuga ulifungua mlango mdogo katikati mwa sakafu, ambapo palikuwa na ngazi iliyoshuka mpaka ndani mwa shimo hii ndogo iliyokuwa na giza. Dorothy ali

Mganga Ajabu Wa Au, utangulizi

Utangulizi  Ngano. masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu jadi. Kila mtoto mdogo mwenye afya anazipenda kwa moyo wake wote hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu. Fari zenye bawa, zilizobuniwa nao Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya watoto kuliko hadithi zote alizobuni mwanadamu. Lakini hadithi hizi zinazohusu fari, zilizohudumuia vizazi sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ katika maktaba ya watoto; wakati umefika kwa hadithi mpya za ajabu nazo zile zilizoeleka za jini,dwafu na fari kuondolewa, pamoja na mambo yote ya kutisha yaliyowekwa na watungaji hadithi ili kutoa funzo. Elimu ya kisasa inawapa watoto maadili; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake. Mtoto huyu anatupilia mbali kwa furaha vitukio vyote asivyokubaliana navyo. Tukiwa na fikra hizi akilini, hadithi ya “ Mganga Ajabu wa Au” iliandikwa kwa lengo moja tu la kuwafurahisha watoto wa siku hii. Hadithi hii inalenga kuwa hadith

Mganga Ajabu wa Au, words search

Search words. Swahili translation of the Wizard of Oz Tafsiri ya Kiswahili  ya kitabu Wizard of Oz Oz in Kiswahili Oz in Swahili Emerald City is Kiswahili Jiji la Zumaridi translation of the wizrd of oz to swahili, kiswahili Has the wizrd of oz been translated into kiswahili? is there a transaltion of the wizard of oz in kiswahili

Swahili translation of the Wonderful Wizard of Oz

Hii ni tafsiri ya kitabu cha L. Frank Baum, The Wonderful Wizard of Oz. Jina lake baada ya kufikiri na kuchunguza maana ya Oz nimeona katika kiswahili ,"Mganga Ajabu Wa Au." Oz lilitokana na ufupisho wa neno Ounce  ambacho ni kipimo cha dhahabu, Kwa ksiwahili ni Aunsi nami nikafupisha likawa Au, ambayo imenipa Mganga Au. I will publish a chapter by chapter of the whole book. Copyright 2011