Tuesday, February 6, 2018

Sura Ya Nne

4. Barabara Iliyopita Msituni.

Baada ya masaa kidogo barabara ikaanza kuwa mbovu, na mwendo ukawa mgumu. Kifukuzakunguru akaanza kujikwa na kuanguka juu ya matofali ya manjano, hapa hayakuwa na mpangilio mwema. Wakati mwingine yalikuwa yamevunjika na kuwa hayapo, na kuacha mashimo ambayo Toto aliruka na Dorothy akaizunguka. Lakini kwa sababu Kifukuzakunguru hakuwa na akili alitembea tu na kuanguka chini kwenye matofali magumu. Hakuumia lakini, Dorothy alimwinua na kumsimamisha huku wakimcheka alivyoanguka.