Utangulizi
Ngano. masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu jadi. Kila mtoto mdogo mwenye afya anazipenda kwa moyo wake wote hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu. Fari zenye bawa, zilizobuniwa nao Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya watoto kuliko hadithi zote alizobuni mwanadamu.
Lakini hadithi hizi zinazohusu fari, zilizohudumuia vizazi sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ katika maktaba ya watoto; wakati umefika kwa hadithi mpya za ajabu nazo zile zilizoeleka za jini,dwafu na fari kuondolewa, pamoja na mambo yote ya kutisha yaliyowekwa na watungaji hadithi ili kutoa funzo. Elimu ya kisasa inawapa watoto maadili; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake. Mtoto huyu anatupilia mbali kwa furaha vitukio vyote asivyokubaliana navyo.
Tukiwa na fikra hizi akilini, hadithi ya “ Mganga Ajabu wa Au” iliandikwa kwa lengo moja tu la kuwafurahisha watoto wa siku hii. Hadithi hii inalenga kuwa hadithi mpya ya kisasa ambapo mambo yote ya furaha yamebakia na yale yote ya kuhuzunisha na kuhusu jinamizi yamewachwa.
L. Frank Baum

Chicago, Aprili, 1900.
Comments
Post a Comment