Skip to main content

Mganga Ajabu Wa Au, Sura ya Pili

2. Kongamano la Dorothy na Watu wa Kushangaza.

Aliamshwa na kishindo kikubwa dorothy asingalikuwa amelala kitandani angeumia. navyo ilivyokuwa kishindo kilimfanya astaajabu na kufikiri kilichofanyika; naye Toto akiiweka pua yake baradi usoni mwake dorothy na whined dismally. Dorothy aliamka na akangalia kila mahali. Nyumba ilikuwa imewacha kusonga; na pia sasa hapakuwa na giza, kwani jua lilikuwa likiwaka kupitia kioo, kujaza chumba chote. Dorothy alitoka kitandani naye toto akimfuata nyuma akiimbia na akaenda akalifungua mlango.
Msichana mdogo aliwika kwa furaha kwa sababu ya mambo yote ya ajabu aliyoyaona macho yake yakipanuka yakawa kubwa kama sahani.

Kimbuga kilikuwa kimeitua nyumba kwa utulivu- kwa kimbuga- katika nchi ya urembo tele. Palikuwa na nyasi yenye rangi ya kijani kibichi nayo miti ilikuwa kubwa na iliyokuwa na matunda makubwa yalionekana tamu sana.Kulikuwa na maua chungu nzima kila mahali alipotazama, ndege wenye rangi ambazo ahakuwahi kuona maisha yake yote yenye urembo wa kupindukia wakiwa wametua mitini. Kwa mbali kidogo kulikuwa na mto mdogo, uliokuwa ukipita katikati ya mimea ilyokuwa pande zote zake, sauti yake ilimfurahisha sana dorothy kawani alikuwa ameishi nchi kavu miaka mingi sana.

Alipokuwa amesimama akitazama urembo huu wote, aliwaona umati wa watu ukija upande wake. Walikuwa watu wa kushangaa ambao hakuwa amewaona maisha yake yote. Hawakuwa wakubwa kama watu wengine ambao alikuwa amewazoea na pia hawakuwa wafupi. Kwa uhakika walikuwa warefu kama dorothy mwenyewe, ingawa dorothy alikuwa mrefu kuliko umri wake, hawa walionekana wazee sana.
Watatu walikuwa wanaume na mmoja alikuwa mwanamke, na wote walikuwa wamevaa mavazi yasiyo ya kawaida. Walivaa kofia duara zilizoinuka kama futi moja juu ya vichwa zao kama pia na kengele ndogo ndogo katika mviringo wa wa kofia ambazo zilitoa sauti nzuri sana walipotembea. Kofia za wanaume zilikuwa rangi ya buluu nayo ya mwanamke ilikuwa nyeupe na alivaa gauni nyeupe iliyokuwa na plaiti kutoka mabegani. Juu yake kulikuwa na nyota ndogo zilimetameta kwenye jua kama almasi. Wanaume walikuwa wamevalia rangi ya manjano kama kofia zao. Wanaume dorothy alifikiri walikuwa wenye umri moja na mjombake dorothy Henri kwani wawili wao walikuwa na ndevu. Lakini mwanamke mdogo alikuwa mzee kuwaliko. Usoni alionekana mzee sana na nywele yake ilikuwa imejaa mvi na alitembea kwa matatizo.

Watu hawa walipokaribia nyumba aliyokuwa amesimama dorothy, walisimam na wakaanza kuzungumza wenyewe kwa wenyewe, wakionekana wakiogopa kukaribia. Lakini mwanamke mfupi alisonga mbele na kumkaribia dorothy na kumwinamia na akazungumza kwa kwa sauti nzuri laini:
"Umekaribishwa ewe mganga mzuri katika nchi ya Munshini. Tuna kushukuru sana ewe mganga mwema kwani umemuua mchawi mwovu kutoka magharibi, na kuokoa na kutuachilia huru kutoka utumwa."

Dorothy alisikiza hotuba hii kwa mshangao. Mwanamke huyu mfupi anamaanisha nini akiimwita mganga, na kusema ya kuwa aliimua mchawi mwovu kutoka mashariki? Dorothy alikuwa msichana mdogo tu. ingekuaje mwanmke huyu akamwita mganga na mwenye nguvu ya kumuua mchawi.Dorothy alijipata tu amabebwa na kimbuga kilomita nyingi kutoka nyumbani; na hakuwa amewahi kuua chochote maisha yake yote.
Lakini mwanamke huyu alionekana akiterejea jibu kutoka kwake; basi Dorothy akasema bila wasiwasi," Wewe ni mkarimu sana , lakini sikuelewi unasema nini. Mimi sijamuua yeyote."
"lakini nyumba yako imefanya hivyo," alisema mwanamke mfupi mzee kwa kicheko," na mambo hayo ni sawa. au onaonaje wewe!' aliendelea akimwonyesha dorothy kona moja ya nyumba." Unaona miguu miwili ikichomoza kutoka chini ya mbao za nyumba.""

Dorothy aliangalia na kutokwa na kilio cha mshangao. Hapo, kwa uhakika, chini ya myumba miguu miwili ilionekana ikichomoka, ikiwa imvalia viatu vya rangi ya fedha.
"Ah! Ah!," alilia Dorothy akiishika mikono kwa mshangao. "Nyumba imemwangukia tatafanya nini?"
"Hakuna chochote cha kufanya ," alisema mwanamke kwa kwa upole.
"Lakini alikuwa nani?" aliuliza Dorothy kwa masikitiko. "Alikuwa mchawi mwovu kutoka mashariki," alimjibu mwanamke mfupi."Mwanmke huyu mwovu alikuwa amewaweka Munchkini katika maisha ya ufungwa kwa miaka mingi amewafanya watumwa wake usiku na mchana. Sasa wamewachiliwa huru kwa hisani yako na wanakushukuru wewe.

"Hawa Munchkini ni akina nani?" Dorothy aliuliza.
"Ni watu wanaoishi katika nchi hii ya mashariki alipotawala mwanamke mlozi."
"Je wewe ni mmoja wa muchkini?" Dorothy aliuliza.
"La , lakini mimi ni rafiki yao, ingawa naishi katika nchi ya kaskazini.
Walipogundua ya kuwa mchawi wa mashariki amekufa ,Muchkini walituma ujumbe nije kwangu nami nikaja mara moja.Mimi ni mganga kutoka magharibi.
"ah!" alilia Dorothy "Wewe pia ni mchawi?"

"la hasha ," alimjibu mwanamke mfupi."Mimi ni mganga mwema anayependwa na watu. Mimi sina nguvu nyingi kama alizokuwa nazo mchawi mwovu aliyetawala , au nami nignweza kuwakomboa watu kwa nguvu zangu."
"Lakini nilidhani yakuwa wachawi wote ni wabaya ," alisema msichana ambaye alikuwa akiogopa kumwona mchawi wa kweli."Ndiyo huo ni ukweli . Kuna na wagnga na wachawi. Huku nchi ya Au kuna waganga wawili wanaoishi kusini na kaskazini, hao ni wale wazuri. Huo ni ukweli kwani mimi ndiye mmoja wao na haiwezi kuwa nimekosea.

Wale wanaoishi mashariki na magharibi ni waovu kabisa , wanawake wawili wachawi; lakini sasa kwa kuwa umemuua mmoja , kunaye tu mchawi mmoja mwovu nchi ya ya au, yule anayeishi magharibi."
"Lakini," alisema Dorothy, baada ya kufikiri kwa muda," Shangazi yangu Em ameniambia ya kuwa wachawi wotewalikufa karne nyingi zilizopita."
"Ni nani huyu shangazi Em?" aliuliza mwanmke mdogomzee.
"Yeye nis hangazi yangu anaishi Kansas nitokapo"
Mganga kutoka kaskazini alionekana akifikiri kwa muda akiwa ameinamisha kichwa chake na macho yake cchini. Kisha akaangalia juu akasema " Sijui huko Kansas ni wapi, kwani sijawahi kukusikia . Je huko utokako ni nchi yenye ustaarabu.

"Ndio," alimjibu Dorothy.
"Basi ndio kwa maana . Huko katika nchi za ustaarabuhakuna waganga, wachawi, wahini na hata walozi. Lakini hapa nchi ya Au, hatujawahi kupata ustarabu, kwani tumefungiwa kutoka nchi zingine za ulimwengu. Hiyo ndio sababu tunao bado waganga na wachawi"
"mnao waganga wanaume?"

"Au mwenyewe ndiye mganga mwenye nguvu sana." alimjibu mwanamke mfupi kwa sauti ya kuogopa." Yeye ananguvu kutuliko sisi sote naye anaishi katika Jiji la Zumaride."
Dorothy alikuwa karibu kuuliza swali lingine , lakini munchkini waliokuwa wamesima wametulia tuli ghafla walipiga nduru wakiwa wanaashiria kwa kidole kona moja ya nyumba alipokuwa amelala mchawi mwovu aliyekufa.

"Ni nini?" aliuliza mwanamke mdogo mzee huku akitazama. Baada ya kuona kilichowashangaza munckini alitoa kicheko.Miguu ya mchawi mwovu ilikuwa imepotea na kuacha tu jivu na viatu vyake vya rangi ya fedha.
"alikuwa ameezeeka sana," alielezea mganga kutoka magharibi," mpaka akakauka chini ya jua kali mpak akwa tu jivu na mchanga. Huo ndio mwisho wake. Lakini viatu vyake vya fedha ni vyako na utavichukua uvalie." Aliinama chini na kuvichukua , baada ya kupanguza vumbi na akampa Dorothy.
"Mchawi kutoka mashariki alivipenda sana viatu hivi vya fedhya," alisema mmoja wa munchkini na pia tumesikia ya kuwa una uchawi unaoandamana na viatu hivyo; lakini hatukuweza kujua ni nini."
Dorothy alivibeba viatu mpak ndani ya nyumba na kuviweka juu ya meza. Akarudi tena kwa Munchkini akasema: " Ningetaka sana kurudi kwa shangazi yangu na mjomba wangu, kwa sababu nina uhakika wanahuzuni juu yangu unaweza kunionyesha njia?"

Muchkini na mganga waliangalina tena wakamtazama Dorothy kisha wakatingiza vichwa vyao kwa huzuni.
"Mashariki, mbali kidogo na hapa," alisema mmoja kuna jangwa kubwa na hakuna anayeweza kulipita akiwa hai.
"Kusini pia shida ni hiyo hiyo," alisema mmoja," kwani, nimeshawahi kwenda huko na kuona. Kusini ni nchi ya wanyama waoitwa Kadili."
"Nimeambiwa," alisema wa tatu,"Magharibi pia mambo ni hayo tu. Nchi hiyo ndipo wanyama waitwao winki wanamoishi, huko ndipo anpotawala Mchawi mwovu wa magharibi, ambaye humfanya mtumwa yeyote apitaye upande huo.

Kaskazini ni nyumbani kwangu," alisema mwanamke mkongwe, " pia huko kumezungukwa na jangwa kama ilivyo nchi yote ya Au. Nian hofia mwanangu itabidi uishi nasi."
Baada ya kusikia haya alianza kulia kwa majonzi, kwa sababu alianza kupatwa na hisia za upweke kwani alikuwa mbali sana kutoka nyumbani na watu hawa asiowajua. Kilio chake kiliwahuzunisha Munchkini waliokuwa na moyo mkarimu, wao pia walitoa vitambaa na wakaanza pia kulia. Mwanamke mzee alitoa kofia yake na akaiweka puani na akaanza kuhesabu," Moja, mbili, tatu" na sauti ya huzuni. Mara tu kofia hiyo ikabadilika na kuwa ubao mdogo uliokuwa umeandikwa kwa chaki nyeupe ujumbe huu:

"Wacheni Dorothy aende jiji la Zumaride."
Mwanamke mzee mdogo alilitoa ubao kutoka puani na baada ya kuyasoma maneno, aliuliza, " Jina lako ni Dorothy ewe mwanangu?"
"Ndio," alijibu mtoto, huku akipanguza machozi yake.
"Basi ni lazima uende katika jiji la Zumaride, Pengine mganga Au atakusaidia."
"Liwapi jiji hili? aliuliza Dorothy.
"Lipo katika nchi inayotawaliwa na Au mwenyewe mganga niliyekuelezea juu yake.
"je , yeye ni mtu mwema?" aliuliza msichana kwa huzuni.
"Yeye ni mganga mwema. Kama yeye ni mwanamume au mwanamke mimi sijui, kwani sijawahi kumwona."
"Nitafika vipi kwake/" aliuliza Dorothy.
"Itakubidi utembee, ni njia ndefu inayopitia nchi ambayo wakati mwingine ni nzuri na yenye giza na mabaya. Lakini nitatumia uganga wangu wote kukulinda kutoka mabaya.
"Uatndamana nami?" aliomba msichana, ambaye kwa sasa alianza kumwona mwanamke huyu mze kama rafiki yake.
"La siwezi," alimjibu,'lakini nitakupa busu langu, na hakuna yeyote atakeyejaribu kudhuru aliye na busu la mganga wa magharibi.

Alikaribi na akambusu Dorothy kichwani. Alipomguza msichana paliwachwa na alama iliyokuwa ikingaaa Dorothy aliigundua hivyo baada ya haya.
Barabara ya kuelekea jiji la zumaride limejengwa kwa mawe ya rangi ya manjano alisema mganga, " Hivyo basi huwezi kupotea. Utakapofika kwake Au usimwogope, mweleze yaliyokufanyikia an umwombe msaada, Kwaheri mwanangu mpendwa,"

Muchkini watatu walimwinamia na wakamtakia safari njema, na baada ya hayo walienda zao kupitia upande wa miti. Mganga alimpungia mkono, akazunguka mara tatu, ghafla akapotelea hakuonekana tene. Toto alishangazwa sana na kupotea kwa mganga huyu.Toto alibweka sana kwani alikuwa amemuogopa sana mganga alipokuwa amesima karibu.
Lakini Dorothy, kwa sababu alijua ya kuwa alikuwa mganga alitarajia aondoke vivyo hivyo na hakushangazwa hata kidogo.

Comments

Popular posts from this blog

Swahili translation of the Wonderful Wizard of Oz

Hii ni tafsiri ya kitabu cha L. Frank Baum, The Wonderful Wizard of Oz. Jina lake baada ya kufikiri na kuchunguza maana ya Oz nimeona katika kiswahili ,"Mganga Ajabu Wa Au." Oz lilitokana na ufupisho wa neno Ounce  ambacho ni kipimo cha dhahabu, Kwa ksiwahili ni Aunsi nami nikafupisha likawa Au, ambayo imenipa Mganga Au. I will publish a chapter by chapter of the whole book. Copyright 2011

Mganga Ajabu Wa Au, sura ya kwanza

MGANGA AJABU WA AU 1. Kimbuga Dorothy aliishi katikati mwambuga kubwa huko Kansas na mjombake Henry aliyekuwa mkulima, pamoja naye shangaziye Em aliyekuwa mkewe mkulima. Nyumba yao ilikuwa ndogo,kwa sababu mbao zilizotumiwa kuitengeneza ilibidi zibebwe maili nyingi. Kulikuwa na kuta nne, sakafu na paa, zilizounda chumba kimoja; chumba hiki kilikuwa na jiko iliyokuwa imejaa kutu, kabati palipowekwa sahani, meza, viti vitatu au vinne, na vitanda. Mjomba Henri na shangazi Em walikuwa na jitanda kona moja, naye Dorothy kijitanda kona nyingine. Hapakuwa na $$$$ hata, pia hapakuwa na $$$ isipokuwa shimo ndogo iliyochimbwa ardhini, iliyoitwa $$$ ya kimbuga, mahali ambapo familia ingekimbia kama mojawapo wa upepo mkubwa ungezuka , iliyokuako kubwa kubwa kiasi cha kuvunja na kuharibu nyumba yoyote pahali popote ilipopita. Ili uingie $$$ ya limbuga ulifungua mlango mdogo katikati mwa sakafu, ambapo palikuwa na ngazi iliyoshuka mpaka ndani mwa shimo hii ndogo iliyokuwa na giza. Dorothy ali

SURA YA KWANZA HADI YA TATU.

Utangulizi     Ngano. masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu jadi. Kila mtoto mdogo mwenye afya anazipenda kwa moyo wake wote hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu. Fari zenye bawa, zilizobuniwa nao Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya watoto kuliko hadithi zote alizobuni mwanadamu.     Lakini hadithi hizi zinazohusu fari, zilizohudumuia vizazi sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ katika maktaba ya watoto; wakati umefika kwa hadithi mpya za ajabu nazo zile zilizoeleka za jini,dwafu na fari kuondolewa, pamoja na mambo yote ya kutisha yaliyowekwa na watungaji hadithi ili kutoa funzo. Elimu ya kisasa inawapa watoto maadili; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake. Mtoto huyu anatupilia mbali kwa furaha vitukio vyote asivyokubaliana navyo.     Tukiwa na fikra hizi akilini, hadithi ya “ Mganga Ajabu wa Au” iliandikwa kwa lengo moja tu la kuwafurahisha watoto wa siku hii. Hadithi hii inalenga kuwa