3. Jinsi Dorothy Alivyomuokoa Kifukuzakunguru Dorothy alipoachwa peke yake alianza kuhisi njaa. Basi akaenda kabatini akajikatia kipande cha mkate kisha akapaka siagi. Alimpa Toto pia mkate, akachukua ndoo na akaenda mtoni kuteka maji. Toto alikimbia mitini ambapo aliwaona ndege na akaanza kuwabwekea. Dorothy alimfuata na hapo mitini aliweza kuona matunda matamu ambayo alichukua kidogo ili ale kama staftahi. Akarudi tena kwenye nyumba na baada ya kutuliza kiu kwa maji matamu ya mto alianza kupanga safari yake ya kuelekea Jiji la Zumaride. Dorothy alikuwa na rinda moja nyingine tu lakini hilo lilikuwa safi na lilikuwa limeanikwa kwenye msumari kando ya kitanda chake. Nalo hili lilikuwa la madoadoa ya rangi ya samawati na nyeupe. Lakini rangi ya buluu ilikuwa imepungua umaridadi wake baada ya kuoshwa mara nyingi, lakini bado ilikuwa nguo nzuri sana. Msichana alinawa kwa uangalifu na kuivalia nguo hio ya bafia yenye madoafoa.Akavalia kofia yake ya kujikinga kutokana na jua iliyokuwa rangi
Influencing Today's Culture and Society