Utangulizi
Ngano, masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu zamani, kila mtoto mdogo mwenye afya huwa na upendo kamili na wa asili kwa hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu na ya dhahiri kuwa si ya kweli. Fairi wenye mabawa wa Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya kitoto kuliko kuliko viumbe vingine vyote vya wanadamu.
Lakini hadithi hizi zinazohusu fairi, zilizotumika kwa vizazi, sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ kwenye maktaba ya watoto; wakati umefika kwa mfululizo mpya wa “hadithi za ajabu” ambazo zimeodolewa dhana za jini, dwafu na fairi, pamoja na mambo yote ya kutisha na ya hofu iliyoundwa na waandishi wao kuashiria maadili ya kutishia kwa kila hadithi. Elimu ya kisasa inajumuisha maadilii; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake za ajabu na kwa furaha huachana na matukio yote yasiyokubalika.
Tukiwa na wazo hili akilini, hadithi ya “Mganga Ajabu wa Au” iliandikwa kwa lengo moja tu la kuwafurahisha watoto wa siku hizi. Inatamania kuwa hadithi mpya ya kisasa, ambamo miujiza na furaha zimebakishwa na yale yote ya kuhuzunisha na kuhusu jinamizi yameachwa.
Chicago, Aprili, 1900.
Comments
Post a Comment