Skip to main content

Posts

Showing posts from 2011

Wasomaji

Kama ungependa kusoma kitabu chote cha Mganga Ajabu Wa Au, nitumie ujumbe nami nitakapomaliza kuitafsiri utakuwa wa kwanza kuipata. Chapisho hili halitakuwa na makosa ya kisarufi kama ilivyosasa.

Mganga Ajabu Wa Au, Sura ya Pili

2. Kongamano la Dorothy na Watu wa Kushangaza. Aliamshwa na kishindo kikubwa dorothy asingalikuwa amelala kitandani angeumia. navyo ilivyokuwa kishindo kilimfanya astaajabu na kufikiri kilichofanyika; naye Toto akiiweka pua yake baradi usoni mwake dorothy na whined dismally. Dorothy aliamka na akangalia kila mahali. Nyumba ilikuwa imewacha kusonga; na pia sasa hapakuwa na giza, kwani jua lilikuwa likiwaka kupitia kioo, kujaza chumba chote. Dorothy alitoka kitandani naye toto akimfuata nyuma akiimbia na akaenda akalifungua mlango. Msichana mdogo aliwika kwa furaha kwa sababu ya mambo yote ya ajabu aliyoyaona macho yake yakipanuka yakawa kubwa kama sahani. Kimbuga kilikuwa kimeitua nyumba kwa utulivu- kwa kimbuga- katika nchi ya urembo tele. Palikuwa na nyasi yenye rangi ya kijani kibichi nayo miti ilikuwa kubwa na iliyokuwa na matunda makubwa yalionekana tamu sana.Kulikuwa na maua chungu nzima kila mahali alipotazama, ndege wenye rangi ambazo ahakuwahi kuona maisha yake yote yen...

Mganga Ajabu Wa Au, sura ya kwanza

MGANGA AJABU WA AU 1. Kimbuga Dorothy aliishi katikati mwa mbuga kubwa huko Kansas na mjombake Henry aliyekuwa mkulima pamoja na shangaziye Em, mkewe mkulima. Nyumba yao ilikuwa ndogo, kwa sababu mbao zilizotumika kuijenga ilibidi zibebwe kilomita nyingi. Kulikuwa na kuta nne, sakafu na paa, zilizounda chumba kimoja. Chumba hiki kilikuwa na jiko iliyokuwa imejaa kutu, kabati iliyowekwa sahani, meza, viti vitatu au vinne na vitanda. Mjomba Henry na shangazi Em walikuwa na jitanda kona moja, naye Dorothy kijitanda kona nyingine. Hapakuwa na dari hata, wala gorofa ya chini isipokuwa shimo ndogo iliyochimbwa ardhini, iliyoitwa  shimo la kimbuga, mahali ambapo familia ingekimbia na kujificha kama mojawapo wa upepo mkubwa ungezuka.Upepo uliokuwa mkubwa kiasi cha kuvunja na kuharibu nyumba yoyote pahali popote ilipopita. Ili uingie shimo la kimbuga ulifungua mlango mdogo katikati mwa sakafu, ambapo palikuwa na ngazi iliyoshuka mpaka ndani ya shimo hii ndogo iliyokuwa na giza. Dorothy a...

Mganga Ajabu Wa Au, utangulizi

Utangulizi  Ngano, masimulizi, hekaya na hadithi nyingine zimekuwa za utotoni tangu zamani, kila mtoto mdogo mwenye afya huwa na upendo kamili na wa asili kwa hadithi hizi kuhusu mambo ya ajabu na ya dhahiri kuwa si ya kweli. Fairi wenye mabawa wa Grimm na Andersen, zimeleta furaha tele katika mioyo ya kitoto kuliko kuliko viumbe vingine vyote vya wanadamu. Lakini hadithi hizi zinazohusu fairi, zilizotumika kwa vizazi, sasa zinaweza kuwekwa katika sehemu ya vitabu vya ‘kihistoria’ kwenye maktaba ya watoto; wakati umefika kwa mfululizo mpya wa  “hadithi za ajabu”  ambazo zimeodolewa dhana za jini, dwafu na fairi, pamoja na mambo yote ya kutisha na ya hofu iliyoundwa na waandishi wao kuashiria maadili ya kutishia kwa kila hadithi. Elimu ya kisasa inajumuisha maadilii; kwa hivyo mtoto wa kisasa anahitaji tu burudani katika hadithi zake za ajabu na kwa furaha huachana na matukio yote yasiyokubalika.   Tukiwa na wazo hili  akilini, hadithi ya “Mganga Ajabu wa Au” i...

Mganga Ajabu wa Au, words search

Search words. Swahili translation of the Wizard of Oz Tafsiri ya Kiswahili  ya kitabu Wizard of Oz Oz in Kiswahili Oz in Swahili Emerald City is Kiswahili Jiji la Zumaridi translation of the wizrd of oz to swahili, kiswahili Has the wizrd of oz been translated into kiswahili? is there a transaltion of the wizard of oz in kiswahili

Swahili translation of the Wonderful Wizard of Oz

Hii ni tafsiri ya kitabu cha L. Frank Baum, The Wonderful Wizard of Oz. Jina lake baada ya kufikiri na kuchunguza maana ya Oz nimeona katika kiswahili ,"Mganga Ajabu Wa Au." Oz lilitokana na ufupisho wa neno Ounce  ambacho ni kipimo cha dhahabu, Kwa ksiwahili ni Aunsi nami nikafupisha likawa Au, ambayo imenipa Mganga Au. I will publish a chapter by chapter of the whole book. Copyright 2011